Naibu waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi William Ole Nasha
Hatua ya ugawaji wa hati hizo kwa kina mama imefikiwa baada ya kukamilika kwa taratibu zote za kisheria zilizofanyika kwa ushirikiano baina ya serikali ya kijiji na asasi ya baraza la wanawake wafugaji.
Wakizungumza mara baada ya kukabidhi hati hizo mkurugenzi wa (PWC), Naomi Lengita, na baadhi ya akina mama wanasema hati hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuwakomboa wanawake wa kimaasai ambao kwa muda mrefu mila na desturi zimekua zikimkandamiza kutokana na mfumo dume ulioota mizizi.
Naibu waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi William Ole Nasha ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Ngorongoro ndiye aliyekabidhi hati hizo anasema asasi hiyo ya kiraia imeonesha nia ya dhati kushirikiana na serikali katika kufikia azma yake ya kuboresha utawala wa ardhi.
Ikumbukwe kuwa kwa miaka iliyopita wanawake wa jamii ya kimaasai hawakuwa na haki hiyo kwa madai kuwa ardhi ni kwa ajili ya wanaume.