Chama Cha Mapinduzi kimewataka wanachama wake wanaopingana na msimamo wa chama hicho kuhusu katiba inayopendekezwa kurudisha kadi na kuondoka mara moja ndani ya chama hicho, badala ya kutumia mgongo ya CCM kuwapotosha watanzania.
Kauli hiyo imetolewa na mjumbe wa kamati kuu wa halmashauri kuu ya taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mh Stephen Wassira, muda mfupi baada ya kupokelewa na wawakilishi wa wananchi wa mkoa wa Mara, ikiwa ni siku chache tu baada ya kumalizika kwa Bunge Maalum la Katiba, ambapo amesema kuna baadhi ya wana CCM wamekuwa wakitumia mgongo wa chama hicho kuwapotosha wananchi kuhusu katiba hiyo inayopendekezwa.
Hata hivyo Mh. Wassira ambaye ni waziri wa nchi ofisi ya Rais mahusiano na uratibu, amesema katiba inayopendekezwa endapo itapitishwa na wananchi itajibu kilio cha miaka mingi kuhusu ukiukwaji wa maadili vikiwemo vitendo vya rushwa ndani ya jamiii.
Chama Cha Mapinduzi kimewataka wanachama wake wanaopingana na msimamo wa chama hicho kuhusu katiba inayopendekezwa kurudisha kadi na kuondoka mara moja ndani ya chama hicho.