Wednesday , 11th Nov , 2015

Wananchi wanaoishi kwenye maeneo ya mabondeni mkoani Iringa wametakiwa kuchukua tahadhari mapema kutokana na mvua kubwa ambazo zinaweza kusababisha madhara makubwa.

Afisa Uhusiano wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Bw. Humphrey Kisika

Afisa uhusiano wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Bw. Humphrey Kisika amesema, wananchi wanaoishi mabondeni waondoke kwa muda ili kupisha mvua za Elnino.

Bw. Kisika amesema, halmashauri imetoa elimu kwa wananchi wake kupitia viongozi wa mitaa na kata ili wananchi wawe na ufahamu wa kutosha.

Bw. Kisika amesema, wapo baadhi ya wanaume wanaoishi mazingira hayo wamefikia hatua ya kutelekeza familia zao kwenye sehemu hatarishi bila kuchukua tahadhari.

Hata hivyo, afisa uhusiano amesema, bora wananchi wachukue tahadhari ya kuondoka kabla ya mvua hizo kuanza kwani baadaye madhara makubwa yanaweza kuwakumba.