Sunday , 6th Mar , 2016

Wakazi wa Jiji la Arusha wamelalamikia ucheleweshaji wa huduma za maabara ambapo wamekua wakikaa muda mrefu kwenye foleni kusubiria huduma hiyo jambo ambalo linasababisha kusimama kwa shughuli nyingine za kijamii na kiuchumi.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Daudi Felix Ntibenda.

Wakizungumzia changamoto hiyo Emma Mollel na Anna Joseph waliofika katika kituo cha Afya cha Karoleni Jijini Arusha,kupata huduma za upimaji wa magonjwa mbalimbali wameiomba serikali iboreshe huduma za maabara ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa na kupunguza msongamano ulioko.

Dokta Luciana Kazimoto ,Daktari wa Hospitali hiyo amesema kuwa wamekua na wakihudumia idadi kubwa ya wagonjwa licha ya changamoto ya uhaba wa vifaa na madawa lakini pia suala la uelewa wa wananchi juu ya vipimo limekua ni dogo hivyo kupelekea mkanganyiko

Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Daudi Felix Ntibenda amesema kuwa tayari wameanza kufanya ukarabati wa vituo vya afya pamoja na uboresha unaofanywa na serikali pamoja na wadau mbalimbali ili kutoa huduma bora za afya kwa wananchi

Uboreshaji wa vituo vya afya vya serikali vilivyoko jijini Arusha huenda ukapungumza msongamano wa watu katika kituo cha afya cha Kaloleni ambacho kinahudumia watu 500 kwa siku idadi ambayo ni kubwa ukilinganisha na miundombinu iliyopo suala ambalo linahitaji upanuzi wa hospitali hiyo.