Monday , 24th Nov , 2014

Wananchi wa kijiji cha Sakila Juu Wilayani Arumeru mkoani Arusha nchini Tanzania wamepinga hatua ya watendaji wa halmashauri ya kugeuza vyumba vya madarasa ya shule yao ya sekondari na kuwa maabara na wametishia kugoma kuchangia.

Moja ya chumba cha darasa kilichogeuzwa Maabara.

Wananchi hao wamesema hatua hiyo inaonesha jinsi mchango na nguvu zao usivyothaminiwa kwani shule wamejenga kwa nguvu zao na walishajenga jengo la maabara linalosubiriwa kupauliwa hivyo hawaoni sababu ya kutumia vyumba vya madarasa na kutoa siku Tano kwa halmashauri hiyo kusitisha zoezi hilo.

Akizungumzia sakata hilo mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Meru Bw. Lucas Malya pamoja na kukiri kuwa uamuzi huo ulipitishwa kwenye vikao amesema walifanya hivyo kwa nia njema ya kutaka kutimiza agizo la Rais.

Diwani wa kata hiyo Bw. Pendael Nasari amekiri kuwa alishiriki kupitisha uamuzi wa kugeuza madarasa ya kusomea wanafunzi kuwa majengo ya maabara na kwamba ulikuwa ni uamuzi wa wajumbe wa kikao kilichopitisha .