Monday , 25th May , 2015

Zoezi la uandikishwaji katika daftari la kudumu kwa mfumo wa BVR limehitimishwa rasmi kwa mkoa wa Mtwara kwa siku ya jana huku changamoto zikijitokeza ikiwemo ya wanafunzi wa sekondari ambao hawajafikisha umri stahiki kujitokeza kujiandikisha.

Waandishi wakiwa katika mazoezi ya uandikishaji kwa mfumo wa BVR.

Akizungumza na East Africa Radio Wakala wa CCM, amewatuhumu wapinzani kwa kusema ndiyo wanaotaka kuwatumia watoto hao kujiandikisha ili waweze kupiga kura katika uchaguzi mkuu.

Kwa upande wake wakala wa CUF amesema kuwa suala hilo siyo la kweli ila ni wasiwasi wa wakala huyo wa CCM ambaye amekuwa na wasiwasi wakati sheria za serikali kwa mtoto aliyezaliwa mwaka 1997 mwezi wa nne hadi wakati wa uchaguzi atakuwa ametimiza miaka 18 ya kupiga kura kisheria.

Naye msimamiza wa uandikishaji huo amesema kuwa wamekumbana na changamoto hiyo lakini walitumia maswali ya kisaikolojia pamoja na kuwataka kupeleka vyeti vya kuazaliwa ili waweze kupata haki yao hiyo.

Kwa upande wake afisa mtendaji wa mtaa huo amesema kuwa changamoto hizo zinazojitokeza ni za kisiasa lakini amethibitisha kuwa zoezi hilo mpaka lilipofikia limekwenda vizuri na hakuna changamoto nyingine zilizojitokeza zaidi ya hizo.