Sunday , 31st Jan , 2016

Walimu wastaafu wa wilaya ya Kongwa wameitaka serikali kuharakisha mafao yao ya uzeeni kwani wanapoyachelewesha wanawafanya kuishi maisha ya taabu baada ya kustaafu.

Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba,

Walimu hao wametoa malalamiko hayo leo kwenye hafla ya kuwaaga walimu wastaafu iliyoandaliwa na Chama Cha Walimu (CWT) Wilaya ya Kongwa ambapo wamesema kuwa mpaka sasa wamefikisha miezi sita tangu wastaafu lakini bado hawajapewa mafao yao.

Wamesema hali hiyo imewafanya kuishi maisha ya taabu kwani kwa kucheleweshewa mafao yao kunawafanya wajione wasio na thamani baada ya kustaafu.

Katibu wa CWT Wilaya ya Kongwa, Pasian Siay amesema kuwa pia kitendo cha serikali kuwacheleweshea wastaafu malipo ya mafao yao ya kustaafu ni changamoto kubwa ambayo inawakabili na kuiomba serikali kulishughulikia suala hilo mapema.