Msangi ambaye pia kitaaluma ni mwalimu ametoa kauli hiyo kwenye hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Walimu (CWT) Wilayani Kongwa kwa ajili ya kuwaaga walimu waliostaafu katika Wilaya hiyo.
Amesema kuna baadhi ya walimu wa kike ambao wamekuwa wakikiuka maadili kwa kuvaa mavazi mafupi na ya kubana wawapo kazini hali ambayo huwa inawanyima wanafunzi wa kiume utulivu wa kujifunza ambapo amewaagiza maofisa elimu kuwaeleza walimu wao namna bora ya uvaaji.
Katika hafla hiyo jumla ya walimu 17 waliostaafu walipata zawadi ya mabati 20 kila mmoja waliyopewa na chyama cha walimu Wilayani humo.

