Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania Bw. Ernest Kimaya akisoma nakala za Katiba Inayopendekezwa yenye maandishi yaliyokuzwa mara baada ya kukabidhiwa.
Aidha Fihanga amesema kuwa swala la kuisoma katiba inayopendekezwa kwa walemavu wote wa mkoa wa Njombe ni muhimu na walipaswa kusoma na kuielewa ambapo hakuna kitabu hata kimoja cha alama za kusoma watu wenye ulemavu wa macho jambo ambalo linaonesha dhahiri kuwa makundi hayo yatashindwa kuipigia kura rasimu hiyo na hayathaminiwi katika jamii.
Kwa upande wake katibu wa chama cha walemavu wasioona Daud Mbanga amesema kuwa haki ya makundi ya watu wenye ulemavu ya kuipigia kura Katiba Inayopendekezwa haitatendeka endapo makundi hayo hayatahusishwa kwenye zoezi la kuipigia kura rasimu hiyo.
Bwana Mbanga amesema kuwa kutokana na makundi hayo kutopata nakala za katiba inayopendekezwa wanatarajia kwenda kwa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe ili kupatiwa ufafanuzi zaidi kwa nini makundi hayo yamesahaulika.
Kwa upande wake wananchi mjini Njombe wamesema kuwa hata wao bado hawajafanikiwa kuisoma Katiba Inayopendekezwa kutokana na nakala kuwa chache jambo ambalo linawafanya watu wengi kushindwa kuisoma yakiwemo makundi ya walemavu.
Katiba pendekezwa inataraji kupigiwa kura ifikapo April 30 licha ya kuwa inategemea kukamilika kwa zoezi la uandikishaji wa wananchi katika daftari la kudumu ambalo mpaka sasa halijakamilika katika mkoa mmoja wa Njombe.