Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi
Agizo amelitoa Mkoani Morogoro ambapo amesema kuwa inadaiwa Migogoro mingi husababishwa na viongozi wa serikali wa ngazi za chini wakiwemo wenyeviti wa vijiji na mitaa kwa kutoa ardhi kinyemela kwa watu wanaojiita kuwa ni wekezaji hivyo kutaka wakuu wa wilaya kuhakikisha wanasimamia na kuendesha vikao vyote vya vijiji vyenye lengo la kutoa ardhi ya zaidi ya hekari 50 kwa mtu binafsi .
Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi amekabidhi vifaa kwa halmashauri ili kuhakikisha wanatoa huduma bora na kodi zote za ardhi kuanzia mwezi ujao kulipwa kwa njia ya kimtandao ili kuongeza kipato kwa hazina na kuondoa mianya ya rushwa huku akiwataka maafisa wa kukabidhi hati ndani ya mwezi mmoja kwa wote wanao maliza kulipia michango yao.