Thursday , 8th Sep , 2016

Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameafikiana kupeana muda wa miezi mitatu hadi Januari mwakani ili kujaribu kutafuta ufumbuzi wa suala la kuridhia ushirikiano wa kibiashara baina ya EAC na Umoja wa Ulaya ujulikanao kama EPA.

Baadhi ya wakuu wa nchi za Afrika Mashariki, muda mfupi kabla ya kikao chao

Akitoa taarifa ya kikao hicho cha dharura kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa EAC, Rais Dk. John Magufuli amekiri kuwa suala la majadiliano ya EPA lilikuwa gumu na limewachukulia muda mwingi wa kikao hicho.

Akiongelea suala la maombi ya Sudan Kusini kupatiwa uanachama wa EAC Rais Dk. Magufuli amesema wakuu wa nchi za Afrika Mashariki wameafikiana kwa pamoja kuridhia uanachama nchi hiyo na sasa kuifanya EAC kuwa na nchi wanachama sita.

Kuhusu Burundi Dk. Magufuli amesema Jumuiya ya Afrika Mashariki imekuwa ikifanya jitihada za kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo chini ya msuluhishi mkuu Rais mstaafu Benjamin Mkapa, na kuitaka jumuiya ya kimataifa kumsaidia kumuwezesha kufanikisha kazi hiyo.