Friday , 17th Apr , 2015

Serikali wilayani butiama mkoani mara imeiagiza bodi ya pamba na makampuni yanayojihusisha na ununuzi wa zao hilo kusimamia kikamilifu kilimo cha mkataba cha zao la pamba ikiwa ni pamoja na kusambaza pembejeo kwa wakati.

Mkuu wa wilaya ya Butiama Bi Annarose Nyamubi.

Hatua ya Usambazaji wa pembejeo hizo umetajwa kuwa utasaidia kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kuinua mchumi kwa mkulima na mkulima kwa ujumla.

Akizungumza na wadau wa zao la pamba,watendaji na viongozi wa serikali wilayani butiama,Mkuu wa wilaya ya Butiama Bi Annarose Nyamubi, amewataka watendaji wa bodi ya pamba pamoja na makampuni ya uchambuzi wa zao hilo kusimamia kilimo hicho cha mkataba ili kiweze kuwanufaishe wakulima wilayani humo na mkoa wa mara kwa ujumla.

Kwa upande wake mratibu wa mfuko wa ufadhili wa kilimo cha mkataba cha zao la pamba nchini TGT, Bw, Donald Sayi, amewaita wadau wote kusimamia kilimo cha mkataba cha zao hilo,kwani amesema hatua itaongeza tija na kuinua hali za wakulima kiuchumi.

Katika kikao hicho imeelezwa kuwa tatizo la kuuzwa kwa fedha tasilimu kwa pembejeo za kilimo badala ya kutolewa kwa mkopo na ucheleweshwaji wa usambazaji wa mbegu aina ya UKM 08 ni miongoni mwa changamoto ambazo zimewakatisha tamaaa wakulima wa zao la pamba katika kilimo cha mkataba wilayani Butiama mkoani Mara.