
Wakili Nabih al-Wahsh, ambaye alitoa kauli hiyo kwenye mahojiano na kituo kimoja cha televisheni alitiwa hatiani kwa kuchochea ubakaji na unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake alisomewa hukumu hiyo akiwa hayuko Mahakamani.
Waendesha mashtaka walidai kauli ya Wakili huyo inahamasisha uvunjifu wa sheria, kutishia amani na kuhatarisha maisha ya raia wa taifa hilo la Kiarabu.
Mahakama pia ilimhukumu Wakili huyo kulipa faini ya dola za kimarekani elfu moja ingawa anaweza kukata rufani.
Wanawake nchini Misri wamekuwa wakikabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia kwa miaka mingi hasa kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watu, na sherehe.