Mkuu wa mkoa wa Lindi, Mwantumu Mahiza
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumalizika kikao cha kamati ya maandalizi ya sherehe hizo jana, Mkuu wa mkoa wa Lindi, Mwantumu Mahiza, amewahasa zaidi wafanya biashara kuto pandisha bei bidhaa zao kwa lengo la kupata faida zaidi.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, amewahasa wakulima wa mkoa huo na wilaya zake kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo ili waweze kujifunza mambo mbalimbali ya kuboresha kilimo kutoka kwa wataalamu wa sekta hiyo.
Aidha kwa mujibu wa Mahiza, maonyesho hayo yanayoadhimishwa kitaifa kwa mwaka wa pili mfululizo mkoani Lindi, yanatarajiwa kufungwa Agosti 8 mwaka huu na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya M. Kikwete.