Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri.
Wakazi hao wamedai kuwa wakati wanajenga nyumba zao katika eneo hilo hawakujua kama ni la shule ya Sekondari ya Wasichana ya Tabora na kwamba kwa sasa hawana mahali pa kwenda.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora, Sipora Liana, amesema wananchi hao ni wavamizi hivyo ni lazima waondoke huku mwanasheria wa serikali ya Mkoa akiwataka wananchi hao kutii sheria za nchi.
Akizungumzia suala hilo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri, amesema hatabadilisha kauli yake mpaka pale wananchi hao watakapokuja na vielelezo vyote vinavyoonyeshwa kukabidhiwa maeneo hayo kihalali na Manispaa ili achuke hatua zaidi dhidi ya watumishi waliowapa viwanja hivyo.