
Athari za mvua jijini Dar es Salaam
Wakizungumza na EATV mara baada ya kushuhudia barabara kadhaa zikiwa hazipitiki baada ya mvua kunyesha na kutuama maji wakazi hao wa jiji wamezitaka halmashauri za jiji kuzingatia ujenzi wa mifereji wanapoingia mikataba na wakandarasi wa kujenga barabara.
Wamesema tatizo hilo limekuwa ni endelevu hata kwa barabara zinazojengwa jambo ambalo wamesema lisiposimamiwa vema kila mwaka mvua zinaponyesha barabara zitakuwa zikijaa maji na kukosa suluhisho la kudumu.