
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassimu Majaliwa amewataka wakandarasi nchini kuungana na wakandarasi wa nje ili waongeze ujuzi na uzoefu, na kuleta ufanisi katika shughuli za uendelezaji miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
Mhe. Majaliwa ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akifungua kongamano la miundombinu baina ya wakandarasi wa ndani na nje na kuongeza kuwa kwakuwa wakandarasi wa nje wanauzoefu wa muda mrefu watawasaidia wale wa ndani kujifunza vitu vingi na baadae kuendeleza miradi mikubwa itakayoachwa na wakandarasi wa nje.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi Muhandisi Edwini Ngonyani amewataka wakandarasi wa ndani kushindana na wale wa nje ili kukuza soko lao ndani na nje ya nchi na kuongeza kuwa wakandarasi watanzania watanufaika na miradi mikubwa ya barabara za juu ambayo itaanza hivi karibuni ambazo zitasaidia kupunguza foleni katika Jiji la Dar es Salaam.