
Mmoja wa wafugaji wa kuku Jijini Arusha.
Hayo yameelezwa na mjasiriamali Boniventura Shiyo anayejihusisha na ufugaji huo, ambaye amesema kuwa kwa sasa biashara hiyo imemuongezea kipato ambacho anakitumia kujiletea maendeleo pamoja na kuendesha familia pasipo kuyumba.
Mjasiriamali huyo amewataka Watanzania kujenga tabia ya uthubutu kwani soko la biashara ya kuku ni kubwa na linazidi kukua kila kukicha.
Hata hivyo Boniventura amesema kuwa kwa sasa anatumuia mashine maalum inayototoa mayai na kuwa vifaranga maarufu kama incubator ambayo imemuongezea fursa ya kuwa muuzaji wa vifaranga pia.
Biashara ya ufugaji wa kuku ni moja kati ya biashara zinazoshamiri kwa kasi katika maeneo mingi nchini hususan maeneo ya mijini ambapo ndipo masoko makubwa yanapatikana kutokana na idadi kubwa ya watumiaji wa bidhaa za mayai na nyama ya kuku.