Baadhi ya bidhaa zilizozlishwa na wajasiriamali wa nchini Tanzania.
Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam Meneja Masoko Afrika Mashariki wa kampuni ya Trufood ya nchini Kenya William Makai amesema kwa miaka mingi bidhaa za Kenya zimekua na ushindani katika soko la kimataifa kuliko zile za Tanzania.
Bw. Makai ameeleza kuwa hali hiyo inasababishwa na baadhi ya wazalishaji wa tanzania kukataa kujifunza kutoka kwa wenzano wa nchi jirani kama kenya na uganda huku akiwataka wafanyabishara na wazalishaji kuyatumia vyema maonyesho ya sabasaba.
Ameongeza kuwa kampuni yake ina zaidi ya miaka 60 ya uzalishaji wa mafanikio ndani ya Kenya na nje ya nchi hiyo ambapo kwa kutumia mifumo mbalimbali imeongeza uzalishaji wa bidhaa bora zinazopendwa na wateja.