Thursday , 3rd Sep , 2015

Katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue amesema wahandisi wazawa wana uwezo mkubwa sawa sawa na wa kutoka nje na wakitumika vizuri watailetea nchi maendeleo na kufikia uchumi wa kati mwaka 2025.

Katibu Mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue

Balozi Sefue ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano wa mwaka wa 13 wa wahandisi ulioandaliwa na Bodi ya Wahandisi nchini ERB na kuongeza kuwa Maendeleo yote duniani huletwa na wahandisi kwani hugusa sekta zote za maendeleo.

Kwa upande wa wizara ya ujenzi kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu wake Eng. joseph Nyamuhangwa amesema bado kuna upungufu wahandisi hapa nchini ili waweze kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika nyanja mbalimbali hapa nchini.

Wakati huohuo Balozi Ombeni Sefue ameshuhudia wahandisi zaidi ya 70 wakila kiapo cha Utii na Uadilifu pamoja na kuwazawadia wahitimu bora wa mwaka 2013/14 na 15.