Wednesday , 25th Jun , 2014

Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la wahamiaji haramu nchini kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki huku nchi ya Burundi ikiongoza kutokana na mahitaji mbalimbali ikiwa ni pamoja na ya kijamii.

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mathias Chikawe.

Akiongea na East Africa Radio,Kaimu msemaji mkuu wa Idara hiyo, Tatu Burhani amesema kutokana na nchi kuwa na mipaka mikubwa udhibiti wa mipaka hiyo imekuwa ni changamoto,kutokana na wananchi wa nchi hizo kuingia nchini kupitia njia za panya.

Bi. Burhani amesema serikali inaendelea kutoa elimu kwa wananchi wa nchi za jirani kufuata sheria na taratibu za kufuata ili kupata vibali kuhamia nchini katika kupata mahitaji muhimu wanayoyakosa katika nchi zao.