Thursday , 30th Jul , 2015

Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania imesema imewakamata zaidi ya watu elfu mbili wasio raia wa Tanzania kwa kosa la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura katika mikoa kumi na tano ya Tanzania,

ambapo kati ya hao watu 60 wakikamatwa Jijini Dar es Salaam ambapo zoezi hilo bado linaendelea.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam katika Makao Makuu ya Uhamiaji na Msemaji Mkuu wa Uhamiaji nchini Tanzania, Abbas Irovya wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu uthibiti na harakati mbalimbali za hali ya uhamiaji na vitendo vya uhamiaji haramu nchini na namna idara yake ilivyendelea kudhibiti mianya ya rushwa