Akitangaza kuanza kwa zoezi hilo Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amewatadhadharisha wagombea watakaokuja kuchukua fomu kwa shamra shamra kuhakikisha wafuasi wao wanakaa umbali wa mita 400 kutoka katika ofisi hizo ili kuepusha vurugu.
Akisisitizi juu ya agizo hilo la NEC, Mkuu wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Kova, amesema jeshi la polisi halitamvumilia mgombea yeyote atakayekiuka agizo hilo na wafuasi wake kusababisha vurugu ama kusababisha baadhi ya shughuli kutofanyika.
Wakati huo huo Jaji Mstaafu Lubuva amekanusha NEC kuhusika na ujumbe unaozunguka mitandaoni unaowataka wananchi kuhakiki taarifa zao za zoezi la BVR kwa kutumia alama ya nyota 152 nyota 00 alama ya reli, na kuwataka wananchi waupuuzie kabisa ujumbe huo.