Akizungumza na Supamix msemaji wa DAWASCO Bi Evalasting Lyaro amesema wananchi hawapaswi kuwa na uwoga wa kuwafichua wezi hao kwani wanahofadhi siri zote za wananchi wanaoshirikiana nao katika kuhahakikisha wanawashuhulikia watu wenye kuhujumu maendeleo ya miundombinu ya maji.
Aidha Bi. Lyaro amesema kuwa wizi wa maji unaofanywa unasababidha shirika hilo kukosa fedha ambazo zingesaidia kuimarisha miondombinu ya shirika hilo na kuongeza mapato.
Mara kwa mara DAWASCO imekuwa ikiwanasa wezi wa maji katika maeneo mengi ambao huwa wamedumu katika wizi huo kwa muda mrefu.

