Monday , 26th Jan , 2015

Chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa(TALGWU) kimetangaza kugomea kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu kama serikali itakuwa haijawalipa madeni yao hadi Julai 31 mwaka huu yanayofikia shilingi 17.

Sehemu ya wafanyakazi wa Serikali za Mitaa

Msimamo huo umetolewa na naibu katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa (TALGWU) nchini Bw. Kibwana Njaa alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa serikali za mitaa mjini Songea na kusema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona serikali halijalipa kipaumbele suala la madeni yao.

Naibu katibu mkuu huyo wa TALGWU anasema wanasikitishwa na jinsi serikali inavyolichukulia suala la madeni yao ya shilingi bilioni17 kwa uzito mdogo.

Wafanyakazi wa serikali za mitaa ambao ni wanachama wa chama hicho wanasema wanaunga mkono msimamo wa chama hicho na kuitaka serikali kulipa madeni yao yakiwemo malimbikizo ya mishahara na pesa za uhamisho.