Thursday , 15th May , 2014

Wafanyakazi wa baadhi ya viwanda mbalimbali binafsi vilivyopo Mtaa wa Dakawa,Chang'ombe Mani

Maji machafu yakitiririka jirani na ukuta wa kiwanda kimoja jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Wafanyakazi wa baadhi ya viwanda mbalimbali binafsi vilivyopo Mtaa wa Dakawa,Chang'ombe Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, wako katika hatari kubwa ya kupata madhara ya kiafya kutokana na maeneo hayo ya viwanda kuzingirwa na maji mengi, machafu na yenye kutoa harufu.

Wakiongea na East Africa Radio jijini Dar es Salaam wafanyakazi wa viwanda hivyo pamoja na wasimamizi wa viwanda, wamesema kuwa hali hiyo imewaletea athari mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusimamisha uzalishaji, na kuibuka kwa magonjwa, hivyo wanaomba serikali na mamlaka husika kuwanusuru na hali hiyo mapema.

Aidha wamezungumzia athari za magonjwa kama vile Dengu, kipindu pindu, na magonjwa ya milipuko kutokana na maji yaliyotuama kati kati ya viwanda hivyo huku kukiwa hakuna jitihada zozote za kuyaondoa.