Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida
Wakiongea katika mkutano wao wa ghafla na mwenyekiti wa eneo hilo wafanyabishara hao wamesema hawana imani na uongozi wa kijiji hicho kutokana na kupokea maelekezo kutoka halmashauri bila kuwashirikisha wao.
Wafanyabiashara hao wamesema kitendo cha kupandisha tozo hiyo ya maegesho kimesababisha madereva wengi wa malori kuacha kuegesha katika eneo hilo kama ilivyo awali hali inayofanya biashara yao kuwa ngumu.
Akitatua mgogoro huo baada ya wananchi kuonesha hasira kali mwenyekiti wa halmashauri ya Iramba bw. Simon Tiosera ameamuru kusitisha ukusanyaji wa kodi wa shilingi 6000 na badala yake waendelee na utaratibu wa kukusanya tozo ya shilingi 3000.