Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro,Mmaiko Waluse .
Hayo yamebainishwa wakati wa mkutano wa wadau wa habari ulioandaliwa na chama cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro MOROPC kwa ufadhili wa umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini UTPC.
Wadau hao wameitaka tume ya taifa ya uchaguzi kuhakikisha wote waliojiandikisha wanapata haki sawa ya kupiga kura, kwa kuandaa utaratibu maalum wa marekebisho ili wajisajili kupiga kura katika maeneo watakayokuwepo tofauti na yale waliyolazimika kujiandikisha kutokana na sababu mbalimbali.
Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro, Mmaiko Waluse amesema taratibu zinafanywa na tume kuhakikisha changamoto zinazoonekana zinatatuliwa huku mwenyekiti wa chama cha wafanya biashara wenye viwanda na kilimo TCCIA mkoa wa Morogoro Bachou Sadiki akiwaasa watanzania kuacha kujichukulia mambo kinyume na taratibu za uchaguzi na kila chombo kina nafasi yake, huku akiwataka viongozi na màmlaka husika kutekeleza vyema wajibu wao kuepuka changamoto zisizo za lazima.