Waziri wa Ardhi, Nyumba na MAendeleo ya Makazi William Lukuvi
Akiongea na waandishi wa habari baada ya kusikiliza baadhi ya madai kati ya madai 120 mwenyekiti wa baraza la ardhi na nyumba wa manispaa ya Ilala Joseph Mlyambina amesema kuna wadaiwa sugu 120 ambao wengi wao ni watu na makampuni binafsi wanaodaiwa mamilion ya fedha za kodi ya Ardhi.
Mlyambina amesema Serikali inategemea kodi kama hizo ili kuwaletea maendeleo wananchi.
kwa upande wa mhasibu mkuu toka wizara ya ardhi Walter Lungu pamoja na mkuu wa kitengo cha kodi Denis Msami wamesema kuwa kulipa kodi ya ardhi ni wajibu wa kila mmiliki wa ardhi na wamedhamiria kutekeleza agizo la waziri wa ardhi William Lukuvi la kuwataka wamiliki wote wa ardhi nchini kulipa ada na kodi zote za ardhi kwa maendeleo ya nchi.
Lungu amesema kwa ujumla idadi kubwa ya wamiliki wa ardhi nchini hawalipi kodi za ardhi wanayoimiliki licha ya sheria kuwataka kufanya hivyo tena kupitia ufafanuzi na maelekezo wanayopewa kila wanapopatiwa hati ya umiliki wa ardhi.
Katika mashauri ya leo kwenye baraza la ardhi wilaya ya Ilala, imebainika kuwa kumekuwa na madai yenye thamani ya kiasi kikubwa cha pesa kwani kati ya mashauri hayo yamo yanayozidi thamani ya fedha za Tanzania shilingi milioni hamsini.