Thursday , 30th Jun , 2016

Baada ya serikali kuwasilisha Bungeni muswada wa marekebisho ya sheria ya ununuzi wa umma ambao umelenga kuziba mianya ya rushwa na matumizi mabaya ya fedha, baadhi ya wanataaluma wa masuala ya uchumi wamesema lengo la sheria hilo ni jambo zuri.

Baada ya serikali kuwasilisha Bungeni muswada wa marekebisho ya sheria ya ununuzi wa umma ambao umelenga kuziba mianya ya rushwa na matumizi mabaya ya fedha za serikali baadhi ya wanataaluma wa masuala ya uchumi nchini wamesema lengo la sheria hiyo inaweza kuwa nzuri au mbaya kutokana na utekelezaji wake utakavyofanyika.

Akizungumza na East Africa Radio Dkt. Abel Kinyondo ambaye ni mchumi na mtafiti kutoka taasisi ya utafiti wa kupunguza umaskini nchini REPOA amesema mabadiliko hayo yamekuja kwa wakati muafaka kwakuwa sheria iliyokuwepo ilikua na mianya mingi ya rushwa hivyo kwa kuwepo kwa sheria mpya ya manunuzi itasaidia sana kupunguza masuala ya ubadhirifu wa fedha za umma.

Amesema sheria peke yake haiwezi ikaondoa matatizo hayo hata hivyo inatakiwa kuhakikisha kunakuwepo na mfumo mzuri wakuondoa kabisa mianya hiyo ya wizi na ubatilifu wa fedha tofauti na uliokuwepo mwanzoni na utekelezaji wake ufanyike kwa uwazi.

Aidha, amesema katika masuala ya ununuzi kuwekwe uwazi ambao kila mtanzania ataona taratibu za manunuzi zinavyokwenda bila kuficha, sheria ihakikishe inawaweka watanzania katika kiwango sawa na kuondoa matabaka,serikali ifanye malipo kwa wakati kwa wazabuni na kuhakikisha sheria inamwangalia mwekezaji wa ndani zaidi ili kuwasaidia wazabuni wadogowadogo waingie katika ushindani wa biashara na kuongeza thamani ya fedha ya Tanzania.