Wednesday , 22nd Jun , 2016

Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson leo amewataka wabunge wa kambi ya upinzani kutoka nje ya bunge haraka kama wanatoka ili shughuli za Bunge ziweze kuendelea kama kawaida.

Dkt. Tulia amefikia uamuzi huo baada ya Bunge kuanza na wabunge wa upinzani kusimama wakitaka kuanza wakitaka kuanza kutoka ndipo Naibu Spika akawataka kama wanatoka wafanye hivyo haraka zaidi.

''Kama mnatoka tokeni haraka ili muokoe muda''-Amesema Naibu Spika Tulia.

Wabunge wa upinzani kwa wiki tatu mfulilizo wameendelea kutoka nje ya bunge na kuacha shughuli za uwakilishi zikiendelea kama kawaida kwa madai ya kutoridhishwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson.

Kwa mujibu wa ajenda yao ambayo waliipitisha wakiongozwa na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni ni kwamba siku yoyote ambayo ataongoza kikao Naibu Spika watakuwa wanatoka nje ya Bunge.