Kiongozi wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi toka nchi za Jumuiya ya Africa Mashariki, Moody Awori.
Awori ambaye amewahi kuwa makamu wa Rais wa Kenya ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam baada ya kuwasili nchini kwa ajili ya kufuatilia namna uchaguzi mkuu utakavyofanyika hapa nchini.
Awori ameongeza kuwa kazi yao kubwa ni kuangalia jinsi ambavyo sheria na taratibu za uchaguzi zinafuatwa na sio kuingilia uchaguzi na mwisho wa uchaguzi wataanda ripoti na kuikabidhi.
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa wizara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Bi. Joyce Mapunjo amesema Tanzania ni nchi ya kidemokrasia ambapo kila baada ya miaka 5 hufanyika uchaguzi na kila baada ya miaka kumi hubadilisha Rais.
Bi. Mapunjo ameongeza kuwa kuna miongozo ya kufuata katika uangalizi wa uchaguzi na waangalizi hao watatakiwa kuifuata.