
Rais wa klabu za waandishi wa habari nchini Tanzania, Kenneth Simbaya.
Akizungumza leo mjini Arusha siku moja kabla ya siku ya Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari hapo kesho, Rais wa Muungano wa Vyama vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Bw. Keneth Simbaya, amesema kuna umuhimu wa kuunganisha nguvu kwa waandishi wa habari kudai sheria hiyo ili kuweza kufanya kazi katika mazingira huru zaidi.
Simbaya amesema pamoja na kuwepo kwa mafanikio mengi nchini ya Uhuru wa habari, lakini waandishi wengi wamejikuta wakikabiliwa na changamoto nyingi, kama vile kutumiwa ujumbe kwa njia ya simu wa kutishiwa maisha yao na baadhi yao kupelekwa mahakamani.
Naye Mhadhiri Mwandamizi wa IJMC Dkt. Ayub Rioba amesema uhuru wa vyombo vya habari umesaidia kubadilisha hulka za baadhi ya watawala waliokuwa wakijiweka nafasi ya Mungu kuwa wao ni kila kitu na sasa nchi zao zimekuwa na maendeleo makubwa tofauti na nyuma.
Wakati huo huo waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam wametoa mitizamo yao kuhusu suala la Uhuru wa Habari nchini na kusema bado kuna sheria kandamizi.