Ustadh Jafari Atiki, kutoka katika taasisi ya Darul Hadith Islamic
Akizungumza jana , Mchungaji Zakaria Lyakungi, kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania, jimbo la Pwani, amesema ni wajibu wa waandishi kuikemea jamii bila woga iwapo kutakuwa na vitendo viovu.
Kwa upande wake, Ustadh Jafari Atiki, kutoka katika taasisi ya Darul Hadith Islamic, amesema waandishi wa habari ni kama viongozi wa dini kwa namna wanavyoaminiwa na jamii, hivyo hawatakiwi kuegemea upande wowote katika ufanyaji wa kazi zao.
Naye, makamu mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC), Jimmy Mahundi, amewasisitiza waandishi kujihepusha kuwa chanzo cha matatizo na baadala yake kuwa msaada kwa jamii inayokumbwa na matatizo na kuhitaji msaada wao.
