Friday , 8th Apr , 2016

Asilimia kubwa ya vituo vya polisi vya Wilaya za Mkoa wa Arusha vinakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa miundombinu na vitendea kazi jambo linaloweza kupunguza kasi ya jeshi la polisi katika kupambana na uhalifu.

Kamanda mteule wa polisi wa mkoa wa Arusha bw Charles Mkumbo,

Miongoni mwa Wilaya zenye hali mbaya zaidi ni pamoja na Longido ambayo aliyekuwa kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas, ambaye anahamia makao makuu anasema mkuu wa kituo na mkuu wa upelelezi wanatumia chumba kimoja kutoa huduma.

Kamanda mteule wa polisi wa mkoa wa Arusha bw Charles Mkumbo, amesema wakati umefika wa halmashauri za wilaya kuvisaidia vituo vya polisi vilivyoko katika maeneo yao.

Akifungua kituo kidogo cha polisi cha Tengeru, Mkuu wa mkoa wa Arusha, Daud Felix Ntebenda, amewaomba watu wenye uwezo wakiwemo wawekezaji kujitolea kusaidiana na wananchi na serikali kuimarisha muindombinu huku akitumia fursa hiyo kuwataka wananchi wanaomiliki silaha bila vibali kuzirejesha.

Wananchi na viongozi wa halmashauri ya Meru, wameendelea kuwalalamikia baadhi ya askari polisi ambao badala ya kuwatumikia raia wamewageuza kuwa vyanzo vya mapato kwa kuwadai rushwa na kuwabambikia kesi na wameiomba serikali kuongeza nguvu kuliboresha jeshi hilo.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, Daud Felix Ntebenda,