Monday , 25th Apr , 2016

Viongozi wa vijiji, kata na tarafa Mkoani Mtwara wametakiwa kujiunga katika Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili kutoa msukumo kwa wananchi wao kuweza kujiunga kwa wingi katika mfuko huo na kuweza kupata matibabu bure.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally,

Hayo yamezungumzwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Mtwara Dkt. Juma Gumbo, wakati akitoa taarifa ya mfuko huo katika kata ya Mayanga, na kudai kuwa ni asilimia 30 ya wakazi wa Mtwara ndio ambao wamejiunga.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, amekiri kuwapo kwa changamoto ya wananchi katika kujiunga na mfuko huo na kudai kuwa hali hiyo kwa kiasi kikubwa inasababishwa na uhaba wa dawa katika zahanti mbalimbali na vituo vya afya jambo ambalo linawafanya wakate tamaa ya kujiunga.

Hata hivyo amesema kutokana na gharama ya uchangiaji kwa mwaka katika mfuko huo kuwa ni sh. 5,000 kwa kaya kiasi ambacho ni kidogo ukilinganisha na mahitaji ya huduma za afya yalivyo kwa sasa, ameamua kuwahamasisha wananchi wakubali kuongeza kiasi hicho na kufikia kati ya sh. 10,000 na 20,000 kwa mwaka.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally,