Wednesday , 9th Dec , 2015

Wananchi wa wilaya ya Morogoro wamewataka viongozi mbalimbali waliochaguliwa kuunga mkono jitihada za Rais Dk John Pombe Magufuli kwa kuhakikisha wanazuia maswala ya rushwa ili kuharakisha utekelezaji na ukamilishaji wa miradi ya maendeleo.

Kaimu mkuu wa wilaya ya Morogoro Bi. Betty Mkwasa

Wakizungumza baada ya kuapishwa kwa baraza jipya la halmashauri ya wilaya ya Morogoro, wananchi hao wamewataka viongozi waliowachagua kuhakiksha wanatilia mkazo suala zima la maendeleo ikiwemo utekelezaji wa miradi na huduma za kijamii ikiwemo maji, zahanatii, barabara na elimu bora na changamoto ya rushwa.

Kaimu mkuu wa wilaya ya Morogoro Bi. Betty Mkwasa amewataka madiwani kushirikiana na wananchi kuhakikisha wanakomesha migogoro ya wakulima na wafugaji, huku mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt.Rajab Rutengwe akisisitiza viongozi wanaochaguliwa kulinda amani ya nchi kwa gharama yeyote

Halmashauri ya wilaya ya Morogoro imemchagua kwa mara nyingine bi Kibena Kingo kuwa mwenyekiti mpya wa baraza hilo la madiwani.