Monday , 5th Jan , 2015

Viongozi wa dini ya kiislam wameombwa kutumia maadhimisho ya Maulidi ya kuzaliwa kwa kiongozi wao Mtume Mohamad S.A.W kwa kuhamasisha jamii hasa vijana kutumia muda na nguvu zao kufanya kazi kwa bidii kuondoa umasikini

Shekhe Mkuu wa mkoa wa Arusha Shabaan Bin Jumaa.

Wakizungumza katika maadhimisho ya sherehe hizo zilizofanyika katika msikiti mkuu wa Ijumaa, mkuu wa mkoa wa Arusha Daud Ntebenda amesema kazi ni sehemu ya ibada na suala la kufanya kazi limepewa kipaimbele na vitabu vyote vitakatifu hivyo ni wajibu wa kila mmoja .

Kwa upande wake Shekhe Mkuu wa mkoa wa Arusha Shabaan Bin Jumaa amesema viongozi wa dini zote hapa duniani pamoja na kubeba ujumbe mkubwa wa kiroho pia wamesisitiza umuhimu wa kila mmoja kufanya kazi pia wameelezea madhara ya kuwepo kwa watu wengi wasiofanya kazi tatizo ambalo linaendelea kuongezeka katika jamii.

Baadhii ya washiriki wa hafla hiyo wakiwemo wawakilishi wa taasisi , mashirika na makampuni binafsi pamoja na kuelezea utayari wao wa kusaidia vijana kupambana na umaskini wamesema asilimia kubwa ya vijana wa sasa hawapendi kufanya kazi ngumu tatizo ambalo linahitaji ushirikiano kulikabili ..