Tuesday , 28th Oct , 2014

Mwenyekiti wa baraza la wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA nchini Tanzania Mh. Halima Mdee amewataka vijana kutotumiwa na wanasiasa wanao lenga kuvuruga amani ya nchi na badalayake watulie ili kujenga taifa lenye amani na utulivu.

Mwenyekiti wa baraza la wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA nchini Tanzania Mh. Halima Mdee.

Mh. Mdee ameyasema hayo baada ya mkutano wa chama hicho kuingia dosari baada ya vijana wanaodaiwa kuwa niwafuasi wa Chama Cha Mapinduzi CCM, kuingia na mabango yao katika mkutano uliokuwa ukifanyika kijiji cha kyamiorwa kata kashalunga wilayani muleba na kusababisha vurugu.

Bi. Halima ameongeza kuwa kwa wale wanaotumwa na mabango watambue kabisa nchi inaendeshwa kwa utawala wa sheria hivyo wanapaswa kuheshimu kwa kile kinachofanyika kisheria na sio kwa kuwa wanatumiwa na watu fulani.

Nao baadhi viongozi wengine wa chama hicho akiwemo mbunge wa viti maalumu Conchester rwamlaza wamewataka wananchi kutoiunga mkono katiba mpya na wakaongeza kuwa wananchi wanatakiwa kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa na kuhakikisha wana chagua viongozi bora ambao wataliongoza taifa hili kwa umakini.