Mwenyekiti wa TACAIDS Dkt. Fatma Mrisho amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akizungumzia maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani Desemba Mosi mwaka huu, ambapo kitaifa nchini Tanzania yataadhimishwa mkoani Njombe, kutokana na mkoa huo kuwa wa kwanza kwa kuwa na idadi kubwa ya waathirika wa ugonjwa wa UKIMWI.
Kwa upande wake mkurugenzi wa sera na mipango wa TACAIDS Dkt. Raphael Kalinga amesema wanakabiliwa na changamoto kwa baadhi ya wagonjwa ambao mara baada ya kugundulika wana virusi vya UKIMWI wanataka kutumia dawa za kufubaza makali ya UKIMWI hata kama kinga ya mgonjwa husika ikiwa bado ipo juu.
wakati huo huo zaidi ya watu milioni 1.6 wanaoishi na virusi vya UKIMWI wamefanikiwa kupata huduma na matunzo, kati yao laki 6.96 walianzishiwa dawa za ARVs baada ya serikali kupokea msaada wa fedha kutoka mfuko wa kimataifa wa kupambana na maradhi ya kifua kikuu, UKIMWI na Malaria.
Akijibu swali la mbunge wa Ole Mhe. Rajab Mbarouk Mohamed aliyeuliza ni kwa namna gani zaidi ya bilioni 155.92 ziliweza kuwasaidia waathirika wa maradhi ya UKIMWI.
Naibu Waziri wa afya na ustawi wa jamii Mhe. Dkt Kebwe Stephen Kebwe amesema fedha hizo zilitumika kutekeleza atua mbalimbali za kudhibiti na kutibu malaria nchini, ambapo amesema utekelezaji wake ulihusisha ununuzi na usambazaji wa vyandarua katika kampeni ya ugawaji vyandarua nchi nzima, dawa mseto, usajili wa maduka muhimu ya dawa pamoja na kuelimisha jamii.
Aidha amesema kupitia fedha hizo serikali ilifanikiwa kufanya tafiti 20 kwa lengo la kuboresha huduma za UKIMWI pamoja na kutoa mafunzo kwa watumishi 1500 wa afya kuhusu jinsi ya kutoa tiba na matunzo.