Naibu waziri wa kazi,vijana na ajira Mheshimiwa Anthony Mavunde amesema serikali imeandaa programu yakuzalisha na kukuza ujuzi kwa watanzania hasa wale wanaohitimu vyuo vikuu na wenginje wa mitaani.
Wazirir mavunde ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na vijana na wajasiliamali nchini na kuongeza kuwa programu ya miaka mitano ambayo inatarajia kuwafikia vijana Milion 4 na laki 4, lengo likiwa ni kuwapa vijana hao ujuzi wa kuwa na sifa zakujiajiri na kuajiriwa.
Amesema mradi huo utawasaidia vijana wengi na wajasiliama nchini kujikwamua kiuchumii na kuongeza pato la taifa kwa kutoa kodi mbalimbali kwenye shughuli zao sambamba na kuwawezesha kupata fulsa za mikopo na mitaji.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi wa World Vision nchini Bwana Anthony Chamungwana amesema hali ya ajira nchini sio nzuri kwakuwa bado takwimu za mwaka 2014 za NBS zinaonyesha asilimia 53 ya vijana bado hawajaajiriwa nchini.

