Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP),Amon Manyama
Akiwasilisha utafiti kutoka shirika hilo,Mhadhri mwandamizi kutoka idara ya uchumi ya chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Wilhelm Ngasamiaku amesema katika nchini zinazoendelea utafiti huo umeleta mafanikio kwa wananchi wake kuondokana na Umasikini.
Dkt. Ngasamiaku amesema mpango huo wa kuwashirikisha vijana wasomi katika maendeleo unaweza kuleta mafanikio iwapo nchi itakuwa na sera zisizokinzana katika utekelezaji wake.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miradi wa UNDP Tanzania, Amon Manyama amesema utafiti huo wameutoa wakati serikali ikiwa katika mikakati ya kuleta maendeleo kupitia uchumi wa viwanda ambao utahusisha zaidi vijana.
Manyama amesema utafiti huo unaonyesha njia ya mipango mbalimbali pamoja na mikakati inayopaswa kutumiwa ikiwemo kutumia vijana wenye elimu ya kati na juu kuviendesha viwanda hivyo kwa kuunganishwa na viwanda vidogo vitakavyojengwa vijijini.