Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya Kayuni amesema jamii inapaswa kuchukua hatua kukabiliana na matumizi ya Madawa ya
kulevya hususani bangi ambayo ameeleza yamekuwa yakiathiri afya za watumiaji hali inayosababisha kuzorota kwa uchumi.
Aidha, Kayuni ametumia nafasi hiyo kuwataka vijana kutumia muda mwingi kufanya kazi kwa bidii kama kauli mbiu ya rais Dokta John Magufuli ya
‘HAPA KAZI TU’ ili kujiletea maendeleo ya kiuchumi na taifa kwa ujumla.







