Thursday , 17th Sep , 2015

Mwanaharakati wa kupinga ubaguzi toka Rwanda Tom Ndahiro amesema kuwa ubaguzi, chuki na maandishi yaliyosababisha wanyarwanda kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Rwanda sasa yanaandikwa hapa nchini.

Mwanaharakati wa kupinga ubaguzi toka Rwanda Tom Ndahiro

Akizungumza katika mkutano wa Jukwaa la Amani linaloangalia namna vyombo vya habari vinavyoweza kulinda au kuvuruga amani hasa wakati wa uchaguzi Ndahiro amesema toka mwaka 2012 kuna baadhi ya viongozi wa dini, wanasiasa na waandishi wa wamekuwa wakiandika makala za kibaguzi zenye kujaa chuki kitu ambacho kina hatarisha amani ya nchi.

Ndahiro ameongeza kuwa lugha za kejeli na dharau dhidi ya jamii fulani mara zote ndio chanzo cha vita vya wenyewe kwa wenyewe kama vilivyotokea nchini Rwanda na kuua maelfu ya wanyarwandwa na hivyo kuwasihi jamii kukemea viashairia hivi vya uvunjifu wa amani.

Aidha Ndahiro amesema kuwa kinga ni bora kuliko tiba na hivyo watanzania wakatae maovu na mambo mabaya ili jamii ibaki salama na kujilinda dhidi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.