Thursday , 17th Mar , 2016

Ripoti mpya ya muungano wa mabunge duniani IPU inaonyesha kuendelea kwa tatizo sugu la kutowakilishwa ipasavyo kwa vijana katika mabunge, wakati huu ambapo idadi ya kundi hilo duniani niikubwa kuliko wakati wowote ule.

Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia kwa Makini Mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika Mkutano wa Wabunge Vijana kutoka Umoja wa Mabunge Duniani (IPU)

Ripoti hiyo iitwayo uwakilishi wa vijana katika mabunge ya kitaifa 2016, iliyozinduliwa leo wakati wa mkutano kuhusu wabunge vijana unaofanyika mjini Lusaka Zambia, imeabaini kwamba ni asilimia 1.9 pekee kati ya wabunge 45,000 wana umri chini ya miaka 30.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa hakuna ongezeko kutokana na utafiti wa IPU wa mwaka 2014 ambapo pia ripoti imeonyesha kuwa karibu theluthi ya mabunge madogo na karibuasilimai 80 ya mabaraza ya seneti hayana hata mbunge mmoja mwenye umri wa chini ya miaka 30.

Hata hivyo ripoti mpya hiyo imetaja nchi ambazo zimepiga hatua katika kuwajumisha vijana katika mabunge yao kuwa ni Sweden, Ecuador, Finland na Norway ambazo zina asilimia 10 au zaidi ya wabunge wenye umri wa chiniya miaka 30.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Mjumbe wa vijana katika Umoja wa Mataifa, Ahmad Alhendawi, amesema kuna haja ya kutafuta njia za kuwashirikisha vijana zaidi, hata kutumia teknohama.