Edward Lowassa akiwa na viongozi wa UKAWA wakati kutangaza kuhamia chama hiko jana katika Hoteli ya Bahari Beach.
Akizungumza leo baada kuchukuwa fomu hiyo katika ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Mtwara Mikindani, Limbakisye Shimwela, Uledi amekiri kuwa bado jimbo hilo lipo katika hali ya sintofahamu juu ya nani anapaswa kuwa mgombea rasmi kupitia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Aidha, amewataka wagombea wa vyama vingine vinavyounda umoja huo kumuunga mkono iwapo UKAWA utamuidhinisha kuwa mgombea rasmi wa jimbo hilo na kwamba hata yeye atafanya hivyo kwa yeyote atakayeidhinishwa.
Akizungumza baada ya kumkabidhi fomu, mkurugenzi wa manispaa hiyo Limbakisye Shimwela, ametoa wito kwa wanasiasa kuepuka na tabia za kugombana katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu na badala yeke wafuate sheria na kanuni zilizopangwa.
Mbali na Jimbo hilo la Mtwara mjini aidha kuna majimbo mengine 13 bado hayajapatiwa ufumbuzi kwa kilE kinachodaiwa ni mivutano ya ni chama gani kinachokubalika katika eneo hilo likiwemo jimbo la Kibamba, Ubungo, Morogoro na mengineyo.