Wednesday , 28th May , 2014

Waziri wa nchi, ofisi ya makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira Dkt. Binilith Mahenge amesema moja ya sababu inayosababisha maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam kufurika maji nyakati za mvua ni kutokana na ujenzi holela unaoziba mikondo ya maji.

Waziri wa nchi, ofisi ya makamu wa Rais - Mazingira, Dkt. Binilith Mahenge.

Akizungumza jijini Dar es salaam na waandishi wa habari juu ya siku ya mazingira duniani Juni 5 mwaka huu, Dkt. Mahenge amesema mpango mkakati wa serikali kwa sasa ni kuhakikisha wale wote waliojenga nyumba katika maeneo hayo wanaondolewa.

Amesema hali hiyo imekuwa ni kero kubwa kwa wananchi kutokana na kujirudia mara kwa mara punde zinaponyesha, huku wananchi wakiwa wanakosa makazi kutokana na maji kukosa njia ya kupita na kuingia katika nyumba zao.