Thursday , 20th Aug , 2015

Serikali imesema ongezeko la ujangili ni chanzo cha kudhoofika kwa sekta ya utalii nchini Tanzania na kudidimiza uchumi wa nchi ambapo matukio ya ujangili kwa kipindi cha miaka 10 yameongeza zaidi na kleta athari kwa Wanyama.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Adelhelm Meru

Hayo yamesemwa na katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelelm Meru na kuongeza kuwa kuna uwezekano ujangili ukaathiri ajira milioni 3.8 kwenye sekta ya utalii katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Dkt. Meru amesema utafiti uliofanywa mwaka jana unaonesha kuwa Tanzania imepoteza zaidi ya nusu ya tembo kutoka 110.000 mwaka 2009 hadi 44,000 huku twiga ambao pia ni alama ya taifa wakipungua kwa kiasi kikubwa.

Ameongeza kuwa Tanzania ina ajira laki saba kutokana na utalii idadi ambayo inaweza kuongezeka mara mbili endapo ujangili ulikothiri kwa wanyamapori utaisha na kukomeshwa kabisa.

Ajira ambazo zitaathirika kutokana na janga hilo ni pamoja na waongoza watalii, madereva, hoteli na wahudumu wa migahawa