
Baadhi ya vijana wakiandaa shamba kwa ajili ya shughuli za kilimo.
Kupitia mradi huo zaidi ya vijana 800 walio vijijini wanatarajiwa kufikiwa na kutapatiwa mafunzo ya nadharia katika sekta ya nishati jadilifu na kilimo, na kwa kuanzia mradi huo utaanza na mikoa minne ambayo ni Arusha, Moshi, Geuta na Kagera.
Akizungumza jijini Dar es salaam leo, Meneja wa mradi huo Bi. Kai Maembe ametoa wito kwa vijana kushiriki na kujitokeza kwa wingi kwa lengo la kuchangamkia fursa hizo za ajira.