Monday , 11th Jul , 2016

Uhaba wa mafuta umeendelea kuwa kero kwa wakazi wa mkoa wa Mtwara ambao wanamaliza wiki sasa wakiwa hawajui ni lini huduma hiyo itarejea katika hali yake ya kawaida,

Mhudumu wa Kituo cha Mafuta ikumuwekea Mteja Mafuta

East Africa Radio imetembelea baadhi ya vitu na kushuhudia foleni ndefu katika kituo cha Total ambacho ndio pekee kinachotoa huduma hiyo katika Manispaa ya Mtwara.

Wamesema hali hiyo inawalazimu kuamka alfajiri kwa ajili ya kuwahi foleni huku wengine wakisafiri umbali mrefu kutoka vijijini na kulazimika kutumia gharama za ziada katika muda wanaosubiri kupata hitaji hilo.

Kwa upande wake, msimamizi wa kituo hicho, Salma Shaibu, amesema katika akiba yao zipo lita elfu kumi ambazo bado wanaendelea kuwauzia wateja huku wakitarajia kupokea mafuta mengine kutoka jijini Dar es Salaam huku akidai kutojua nini kinapeleka uhaba huo.